Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 118. Kufikiwa na Kushiriki kwa Umma

(1) Bunge–

  • (a) litafanya shughuli zake kwa njia ya uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na
  • (b) litarahisisha kushiriki na kuhusishwa kwa umma katika shughuli za kutunga sheria na shughuli nyingine za Bunge na kamati zake.

(2) Bunge halitazuia umma au chombo chochote cha habari dhidi ya kuhudhuria vikao isipokuwa katika hali mahususi ambazo Spika husika ataamua kwamba kuna sababu za kuridhisha kufanya hivyo.