Kifungu 117. Mamlaka, Haki na Kinga za Bunge
Kutakuwa na uhuru wa kujieleza na kujadili Bungeni.
Kifungu 118. Kufikiwa na Kushiriki kwa Umma
Bunge litafanya shughuli zake kwa njia ya uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma.
Kifungu 119. Haki ya Kulalamikia Bunge
Kila mtu ana haki ya kulalamikia Bunge ili lishughulikie suala lolote lililo katika mamlaka yake.
Kifungu 120. Lugha Rasmi za Bunge
Lugha rasmi za Bunge zitakuwa Kiswahili, Kiingereza na lugha ya ishara.
Kifungu 121. Idadi ya Wabunge Katika Vikao
Idadi katika Bunge itakuwa wabunge hamsini katika Baraza la Kitaifa na wabunge kumi na tano katika Seneti.
Kifungu 122. Kupiga Kura Bungeni
Mbunge hatapigia kura suala ambalo yeye mwenyewe ana maslahi ya kifedha.
Kifungu 123. Maamuzi ya Seneti
Wakati Seneti itakapopigia kura kuhusiana na suala lolote isipokowa Mswada, Spika ataamua iwapo suala hilo linaathiri au kutoathiri kaunti.
Kifungu 124. Kamati na Kanuni za Kuendesha Bunge
Kila Bunge linaweza kubuni kamati, na kuweka kanuni za kuendesha Bunge ili kusimamia shughuli zake ikiwa ni pamoja na shughuli za kamati zake.
Kifungu 125. Uwezo wa Kuitisha Ushahidi
Bunge lolote na kamati yoyote yake, lina uwezo wa kumuita mtu yeyote kwa kusudi la kutoa ushahidi mbele yake.