Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 119. Haki ya Kulalamikia Bunge

(1) Kila mtu ana haki ya kulalamikia Bunge ili lishughulikie suala lolote lililo katika mamlaka yake ikiwa ni pamoja na, kurekebisha au kutoa sheria yoyote.

(2) Bunge litaweka Vifungu vya muhimu kuhusu utaratibu wa kutekeleza haki hii.