Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 77. Vizuizi Katika Shughuli za Maafisa wa Serikali

(1) Afisa wa Serikali ambaye ni mtumishi wa kudumu hatashiriki kazi nyingine yoyote ya kulipwa.

(2) Afisa yeyote wa Serikali wa kuteuliwa hatashikilia afisi ya chama cha kisiasa.

(3) Afisa wa Serikali aliyestaafu na anayepokea malipo ya uzeeni kutoka katika fedha za umma, hatakubali zaidi ya nyadhifa mbili za kulipwa mshahara kwa wakati mmoja kama mwenyekiti, mkurugenzi au mwajiriwa wa–

  • (a) kampuni inayomilikiwa au kudhibitiwa na Serikali; na
  • (b) idara ya Serikali.

(4) Afisa wa Serikali aliyestaafu hatapokea mshahara kutoka katika fedha za umma isipokuwa kama inavyoelezwa katika ibara ya (3).