Kifungu 73. Majukumu ya Uongozi
Mamlaka yaliyotolewa kwa afisa wa Serikali ni amana ya umma.
Kifungu 74. Kiapo cha Uaminifu kwa Maafisa wa Serikali
Kabla ya kuhudumu katika afisi ya serikali kila mtu aliyechaguliwa au kuteuliwa katika afisi ya Serikali ataapa.
Kifungu 75. Mienendo ya Maafisa wa Serikali
Afisa wa Serikali atakuwa na mienendo iliyonyooka katika maisha yake ya kuhudumia umma.
Kifungu 76. Uadilifu wa Kifedha kwa Maafisa wa Serikali
Zawadi au mchango wowote kwa afisa wa Serikali katika shughuli za umma au rasmi, itakuwa zawadi kwa Jamhuri.
Kifungu 77. Vizuizi Katika Shughuli za Maafisa wa Serikali
Afisa wa Serikali ambaye ni mtumishi wa kudumu hatashiriki kazi nyingine yoyote ya kulipwa.
Kifungu 78. Uraia na Uongozi
Hakuna mtu anayepaswa kuchaguliwa au kuteuliwa katika afisi ya Serikali ikiwa si raia wa Kenya.
Kifungu 79. Sheria ya Kuundwa kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi
Bunge litatunga sheria ya kubuniwa kwa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi.
Kifungu 80. Sheria Kuhusu Uongozi
Bunge litatunga sheria kubuni taratibu na mikakati ya kutekeleza sura hii kwa njia ifaayo