Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 80. Sheria Kuhusu Uongozi

Bunge litatunga sheria–

  • (a) kubuni taratibu na mikakati ya kutekeleza sura hii kwa njia ifaayo;
  • (b) kupendekeza adhabu zaidi ya zile zinazotajwa katika Kifungu cha 75, ambazo zinaweza kuamriwa kwa sababu ya kutofuata maagizo ya Sura hii;
  • (c) kusaidia katika utekelezaji wa Sura hii pakiwa na marekebisho yanayofaa kwa maafisa wa umma; na
  • (d) kuunda masharti mengine yoyote katika kuhakikisha udumishaji wa kanuni za uongozi na uadilifu ambayo yametajwa katika Sura hii, na utekelezaji wa masharti ya Sura hii.