Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 76. Uadilifu wa Kifedha kwa Maafisa wa Serikali

(1) Zawadi au mchango wowote kwa afisa wa Serikali katika shughuli za umma au rasmi, itakuwa zawadi kwa Jamhuri na itakabidhiwa Serikali isipokuwa ikiidhinishwa na au chini ya Sheria ya Bunge.

(2) Afisa wa Serikali–

  • (a) hatamiliki akaunti ya benki nje ya Kenya isipokuwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge; au
  • (b) hataomba au kukubali mkopo au manufaa ya kibinafsi katika hali zinazotatiza uadilifu wake.