Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 69. Kanuni na Wajibu Kuhusiana na Mazingira

(1) Serikali–

  • (a) itahakikisha matumizi, usimamizi, na uhifadhi wa mazingira na maliasili unaodumishwa na kuhakikisha usawa katika ugavi wa faida zinazopatikana.
  • (b) itafanya juhudi ili kutimiza na kuhakikisha kuwa angalau asilimia kumi ya ardhi ya Kenya imepandwa miti;
  • (c) italinda na kukuza hakimiliki za rasilmali za kiakili na elimu ya jadi ya uanuwai wa viumbe na rasilmali za kinasaba za kuzaliwa za jamii;
  • (d) itahimiza kushiriki kwa umma katika usimamizi, utunzaji, na uhifadhi wa mazingira.
  • (e) italinda rasilmali zote za kinasaba na uanuwai wa kielimu viumbe;
  • (f) itaanzisha mifumo ya kutathmini athari ya mazingira, ukaguzi wa mazingira na usimamizi wa mazingira hayo;
  • (g) itatupilia mbali michakato na shughuli ambazo zinaweza kuhatarisha mazingira; na
  • (h) kutumia mazingira na maliasili kwa manufaa ya Wakenya.

(2) Kila mtu anawajibika kushirikiana na idara za Serikali na watu wengine kulinda na kuhifadhi mazingira na kuhakikisha kuna maendeleo ya kiekolojia na matumizi ya rasilmali.