Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 71. Makubaliano Kuhusiana na Maliasili

(1) Mapatano yoyote yanaweza kuidhinishwa na Bunge iwapo-

  • (a) yanahusisha utoaji wa haki au makubaliano na, au kwa niaba ya mtu yeyote, ikiwemo Serikali ya taifa kwa mtu mwingine, ya kutumia maliasili yoyote iliyo nchini Kenya; na
  • (b) yataafikiwa siku ya kuanza kutumia Katiba hii au baadaye.

(2) Kupitia utungaji wa sheria, Bunge litatoa viwango vya maafikiano yatakayoidhinishwa chini ya ibara ya (1).