Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 10. Maadili ya Kitaifa na Kanuni za Utawala

(1) Maadili ya kitaifa, kanuni na malengo yaliyo katika Sura hii yatazingatiwa na idara mbalimbali za Serikali, watumishi wa umma na watu wote wanapo–-

  • (a) tekeleza au kufasiri Katiba hii;
  • (b) tumia, tekeleza au kufasiri sheria yoyote; au
  • (c) tunga, au kutekeleza maamuzi kuhusu sera ya kitaifa.

(2) Maadili ya kanuni za uongozi ni pamoja na-–

  • (a) uzalendo, umoja wa kitaifa, kushirikiana na ugatuzi wa mamlaka, utawala wa sheria, demokrasia na kushiriki kwa watu;
  • (b) heshima ya binadamu, usawa, haki za jamii, kushirikishwa, haki za binadamu, kutobagua na kulindwa kwa makundi yaliyotengwa.
  • (c) utawala mwema, uadilifu, uwazi na uwajibikaji; na
  • (d) maendeleo endelevu.