(1) Lugha ya taifa ya Jamhuri ni Kiswahili.

(2) Lugha rasmi za Jamhuri ya Kenya ni Kiswahili na Kiingereza.

(3) Serikali–

  • (a) Itakuza na kulinda lugha tofauti za wananchi wa Kenya; na
  • (b) Italinda na itastawisha matumizi ya lugha za kiasili, Lugha Ishara ya Kenya, Breli na njia nyingine za mawasiliano na teknolojia zinazoweza kufikiwa na watu wenye ulemavu.