Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Serikali ya Kitaifa

(Mamlaka na kazi za serikali ya kitaifa—)

  1. Mashauri ya kigeni, sera ya kigeni, na biashara ya kimataifa.
  2. Matumizi ya maji ya kimataifa na rasilimali za maji.
  3. Uhamiaji na uraia.
  4. Uhusiano kati ya dini na serikali.
  5. Sera ya lugha na ukuzaji wa lugha rasmi na lugha za kiasili.
  6. Ulinzi wa kitaifa na matumizi ya huduma za ulinzi za kitaifa..
  7. Huduma za polisi , pamoja na—
    (a) Kuweka viwango vya kuajiri, mafunzo kwa polisi na matumizi ya huduma za polisi;
    (b) Sheria ya jinai; na
    (c) Huduma za Marekebisho.
  8. Mahakama.
  9. Sera ya kitaifa ya uchumi na mipango.
  10. Sera ya fedha, sarafu, benki (pamoja na benki kuu) kuanzishwa pamoja na usimamizi wa shughuli za benki, bima na mashirika ya kifedha.
  11. Takwimu za kitaifa na data kuhusu idadi ya watu, uchumi na jamii kwa jumla.
  12. Haki miliki
  13. Viwango vya utendakazi.
  14. Ulinzi wa watumiaji, pamoja na viwango vya usalama wa kijamii na mipango ya kitaalamu ya kustaafu.
  15. Sera ya Elimu, viwango, Mitalaa, mitihani, na utoaji wa hati za vyuo vikuu.
  16. Vyuo Vikuu, taasisi za mafunzo ya kati na taasisi nyingine za utafiti na masomo ya juu na shule za msingi, elimu maalumu, shule za upili na vyuo vya elimu maalumu.
  17. Ukuzaji wa michezo na elimu ya michezo.
  18. Uchukuzi na mawasiliano, pamoja na, hasa—
    (a) Usafiri wa barabara;
    (b) Ujenzi na matumizi ya barabara kuu za kitaifa;
    (c) Viwango vya ujenzi na uhifadhi wa barabara zingine za kaunti;
    (d) Reli;
    (e) Mifereji ya mabomba;
    (f) Usafiri wa baharini;
    (g) vyombo vya anga vinavyotumiwa na raia;
    (h) Usafiri wa angani;
    (i) Huduma za posta;
    (j) Mawasiliano ya simu, redio na runinga na;
    (k) matangazo ya redio na runinga.
  19. Huduma ya kitaifa ya kazi za umma.
  20. Sera ya nyumba.
  21. Kanuni za kijumla za mipango ya ardhi na ushirikishaji wa mipango na kaunti.
  22. Uhifadhi wa mazingira na maliasili kwa mpango wa kuanzisha mfumo wa maendeleo endelevu, pamoja na, hasa—
    (a) Uvuvi, usasi na ukusanyaji;
    (b) Ulinzi wa wanyama wa kufugwa na wanyama pori;
    (c) Uhifadhi wa maji, kuhifadhi wa mabaki ya maji, uhandisi unaohusu maji na usalama wa mabwawa; na
    (d) Sera ya kawi
  23. Hospitali za Kitaifa.
  24. Usimamizi wa majanga.
  25. Minara ya zamani ya kihistoria yenye umuhimu wa kitaifa.
  26. Chaguzi za kitaifa.
  27. Sera ya Afya.
  28. Sera ya Kilimo.
  29. sera ya utatibu wa mifugo.
  30. Sera ya kawi pamoja na nguvu za umeme, mtandao wa gesi, na usimamiaji wa kawi.
  31. Ujenzi wa utendakazi na usaidizi wa kiufundi katika kaunti
  32. Uwekezaji wa umma.
  33. Uwekaji dau wa kitaifa, makasino na aina mbalimbali za uchezaji kamari.
  34. Sera ya utalii na maendeleo.