Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kiapo cha Spika/Naibu wa Spika wa Seneti/Baraza Kuu la Kitaifa

Mimi ,……………….. , nikiwa nimechaguliwa kama Spika/ Naibu wa Spika wa Seneti/ Baraza Kuu la Kitaifa ninaapa kwamba(kwa jina la Mwenyezi Mungu) (nakubali kwa dhati) kwamba nitakuwa mwaminifu kwa watu na Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatekeleza kwa uaminifu na uangalifu kazi zangu kama Spika/Naibu wa Spika wa Seneti/Baraza Kuu la Kitaifa; kwamba nitatii, nitaheshimu, nitatea, nitahifadhi, nitalinda na kuitetea Katiba hii ya Jamhuri ya Kenya; na kwamba nitafanya haki kwa watu wote kulingana na Katiba hii ya Kenya na sheria na desturi za Bunge bila woga au upendeleo, upendo au chuki. (Ee Mungu nisaidie).