Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kiapo/Kukiri kuwa Mbunge (Seneti/Baraza Kuu la Kitaifa)

Mimi,……………………, nikiwa nimechaguliwa mwachama wa Seneti/Baraza Kuu la Kitaifa ninaapa (Kwa jina la Mwenyezi Mungu) (ninathibitisha kwa dhati) kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa Watu na Jamhuri ya Kenya; kwamba nitatii, kuheshimu, kutetea, kulinda na kuhifadhi Katiba ya Jamhuri ya Kenya; na kwamba nitatekeleza majukumu yangu ya ubunge kwa uaminifu na uangalifu. (Ee Mungu nisaidie).