Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Viapo kwa Jaji mkuu/Rais wa Mahakama Kuu, Majaji wa Mahakama Kuu, Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama ya Juu

Mimi, ……………………, (Jaji Mkuu /Rais wa Mahakama Kuu, jaji wa Mahakama Kuu, jaji wa Mahakama ya Rufani, jaji wa Mahakama ya Juu) nina (apa kwa jina la Mwenyezi Mungu)/(nakubali kwa dhati) kutumikia watu wa Jamhuri ya Kenya na kutekeleza haki bila mapendeleo kulingana na Katiba hii na kwa sheria zilizowekwa, na sheria na desturi za Jamhuri, bila woga wowote, upendeleo, ubaguzi, upendo, chuki, ama athari ya kisiasa, kidini, ama ushawishi wowote. Katika kutekeleza majukumu ya kisheria ambayo nimepewa, kwa uwezo wangu wote, na kwa wakati wangu wote, nitalinda, nitasimamia, na kutetea Katiba hii kwa ajili ya kulinda hadhi na heshima ya mahakama na mfumo wa mahakama za Kenya na kukuza haki, uhuru, uwezo na uadilifu ndani yake. (Ee Mungu nisaidie).