Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 145. Kuondolewa kwa Rais Kupitia kwa Kura ya Kutokuwa na Imani

(1) Mwanachama wa Baraza la Kitaifa, iwapo ataungwa mkono na thuluthi moja ya Wabunge wote, anaweza kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Rais–

 • (a) kwa misingi ya ukiukaji mkubwa wa Vifungu vya vya Katiba hii na na sheria nyingine yoyote.
 • (b) ikiwa pana sababu kubwa za kuamini kwamba Rais amehusika katika uhalifu kulingana na sheria za kitaifa au kimataifa;au
 • (c) utovu mkubwa wa nidhamu.

(2) Iwapo thuluthi mbili ya Wabunge wote wataunga mkono hoja chini ya ibara ya (1)–

 • (a) Spika atamuarifu Spika wa Seneti kuhusu uamuzi huo katka muda wa siku mbili; na
 • (b) Rais ataendelea kutekeleza majukumu ya afisi ikisubiriwa matokeo ya mashauri yanayohitajika katika Kifungu cha hiki.

(3) kwa kipindi cha siku saba baada ya kupokea maamuzi kutoka kwa Spika wa Baraza la Kitaifa–

 • (a) Spika wa Seneti ataandaa mkutano wa Seneti ili kusikia mashtaka dhidi ya Rais;
 • (b) Baraza la Seneti, kwa uamuzi wake, linaweza kuteua kamati maalum itakayohusisha watu kumi na moja kati yao ili kuchunguza suala hili.

(4) Tume hii maalum iliyochaguliwa chini ya ibara ya (3) (b)–

 • (a) itachunguza suala hilo; na
 • (b) kisha kwa muda wa siku kumi kuripoti kwa Seneti ikiwa imepata tuhuma dhidi ya Rais ambazo zinaweza kuthibitishwa.

(5) Rais wa ana haki ya kwenda au kuwakilishwa mbele ya tume hii maalum wakati wa uchunguzi .

(6) Iwapo kamati maalum itaripoti kuwa yale yaliyomo katika tuhuma dhidi ya Rais -

 • (a) hayajathibitishwa, hakuna mashtaka zaidi yatayowasilishwa chini ya Kifungu cha hiki yanayohusiana na tuhuma hizi.
 • (b) yamethibitishwa, basi baraza la Seneti, baada ya kumpa Rais nafasi ya kusikilizwa, litapigia kura mashtaka ya kutokuwa na imani.

(7) Na iwapo theluthi mbili ya wanachama wa Seneti watapiga kura kushikilia mashtaka ya kutokuwa na imani na Rais, basi atakoma kushikilia mamlaka ya afisi yake kama Rais wa nchi.