Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 143. Kulindwa Dhidi ya Kufunguliwa Mashtaka

(1) Mashtaka yoyote ya jinai hayatafunguliwa au kuendeshwa katika mahakama yoyote dhidi ya Rais au yeyote ambaye anashikilia afisi ya Rais wakati wa hatamu ya uongozi wake.

(2) Mashtaka ya kesi za madai hayatawasilishwa katika mahakama yoyote dhidi ya Rais au yeyote anayetekeleza majukumu ya afisi hiyo wakati wa hatamu yake kutokana na chochote anachokifanya au kutofanya katika kutekeleza mamlaka yake yaliyo kwenye Katiba hii.

(3) Pale ambapo masharti katika sheria yanawekewa mipaka ya wakati ambao mashtaka haya yanaweza kuwasilishwa dhidi ya mtu huyu kwa mujibu wa Ibara ya (1) au (2), wakati ambapo mtu huyuanashikilia au kutekeleza majukumu ya afisi ya Rais hakitazingatiwa katika kuhesabu wakati ambao unaelezewa na sheria hii.

(4) Kinga dhidi ya kushtakiwa kwa Rais iliyo katika Kifungu cha hiki, haitatumika kwa hatia ambazo Rais anaweza kushtakiwa chini ya mkataba wowote ambao Kenya ni mshiriki na ambao unapinga kinga kama hii.