Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 42. Mazingira

Kila mtu ana haki ya kuishi katika mazingira safi na salama, ambapo ni pamoja na haki ya–

  • (a) kutunziwa mazingira kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo kupitia kwa hatua za kisheria na nyinginezo hasa zile ambazo zinakusudiwa katika Kifungu cha 69;
  • (b) Kuhakikisha kuwa wajibu unaohusu mazingira, ulio chini ya Kifungu cha ya 70 umetimizwa.