Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 43. Haki za Kiuchumi na Kijamii

(1) Kila mtu ana haki ya–

  • (a) kupata kiwango cha juu kabisa kinachowezekana cha afya, kinachohusu haki ya huduma za malezi ya kiafya ikiwa ni pamoja na malezi ya afya ya uzazi;
  • (b) kupata makao ya kuridhisha, na viwango vinavyostahili vya usafi
  • (c) kutokuwa na njaa, na kupata chakula cha kutosha na kinachostahili;
  • (d) kupata maji safi na salama na ya kutosha;
  • (e) usalama wa kijamii ; na
  • (f) elimu.

(2) Mtu hatanyimwa matibabu ya dharura.

(3) Serikali itatoa ulinzi wa kijamii unaofaa kwa wale ambao hawawezi kujisimamia wao wenyewe na jamii zao.