Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 41. Mahusiano ya Kikazi

(1) Kila mtu ana haki ya kanuni sawa za kikazi.

(2) Kila mfanyakazi ana haki ya–

  • (a) kulipwa ipasavyo;
  • (b) mazingira ya kufaa ya kufanyia kazi;
  • (c) kuunda, kujiunga au kushiriki katika shughuli na mipango ya vyama vya wafanyakazi; na
  • (d) kugoma.

(3) Kila mwajiri ana haki ya–

  • (a) kuunda au kujiunga na vyama vya waajiri; na
  • (b) kushiriki katika shughuli na mipango ya vyama vya waajiri.

(4) Kila chama cha wafanyakazi na vyama vya waajiri vina haki ya–

  • (a) kuamua usimamizi wake, mipango na shughuli zake;
  • (b) kupanga; na
  • (c) kuunda na kujiunga na shirikisho.

(5) Kila chama cha wafanyakazi, muungano wa wajiri na mwajiri wana haki ya kushiriki katika maafikiano ya pamoja.