Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 26. Haki ya Kuishi

(1) Kila mtu ana haki ya kuishi.

(2) Maisha ya mtu huanza baada ya kutunga mimba.

(3) Mtu hatauawa kimaksudi, isipokuwa kwa kiwango kinachoidhinishwa na Katiba hii au kwa sheria nyingine iliyoandikwa.

(4) Uavyaji mimba hauruhusiwi, isipokuwa kwa maoni ya mtaalamu wa masuala ya afya, kuna haja ya matibabu ya dharura, au maisha au afya ya mama imo hatarini au kwa kuidhinishwa na sheria nyingine iliyoandikwa.