Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 25. Haki na Uhuru Usioweza Kuwekewa Mipaka

Licha ya sharti lolote lingine katika Katiba hii, hakutakuwa na mipaka dhidi ya haki na uhuru wa kimsingi ufuatao–

  • (a) uhuru dhidi ya mateso, unyanyasaji au adhabu zilizokiuka ubinadamu;
  • (b) uhuru dhidi ya utumwa;
  • (c) haki kwenye kesi ; na
  • (d) haki ya kuitikia amri ya kufikishwa mahakamani.