Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 29. Uhuru na Usalama wa Mtu

Kila mtu ana haki ya uhuru na usalama wake unaohusisha haki ya–

  • (a) kutonyimwa uhuru kiholela bila sababu;
  • (b) kutozuiliwa bila kushtakiwa mahakamani, isipokuwa wakati wa hali ya hatari ambapo kifungo cha aina hiyo kinaelezwa katika Kifungu cha 58;
  • (c) kuwa huru dhidi ya aina zote za ghasia kutoka kwa umma au watu binafsi;
  • (d) kutoteswa kwa njia yoyote ile, iwe ya kimwili au kiakili;
  • (e) kutopewa adhabu ya viboko; au
  • (f) kutotendewa au kupewa adhabu za kikatili, kudhalilisha au kushusha hadhi ya ubinadamu.