Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 172. Majukumu ya Tume ya Huduma za Mahakama

(1) Tume ya Huduma za Mahakama itahakikisha na kuimarisha uhuru na uwajibikaji wa idara ya Mahakama na kuimarisha uhuru na uwazi wa mahakama na usimamizi bora na wenye uwazi na haki pamoja na–

  • (a) kupendekeza kwa Rais wa Taifa watu wa kuteuliwa kuwa majaji;
  • (b) kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masharti ya utendajikazi wa–
    • (i) majaji na maafisa wengine wa mahakama kando na mishahara; na
    • (ii) wafanyikazi wa mahakama; kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu hali na mazingira ya utendajikazi wa wafanyakazi katika idara ya mahakama;
  • (c) kuteua, kupokea malalamiko ya kupinga, kuchunguza na kuwafuta au hatua nyinginezo za kuwaadhibu, kuwasajili,mahakimu na maafisa wengine wa mahakama na wafanyakazi wengine wa mahakamani, kwa njia ambayo imetolewa na Sheria ya Bunge.
  • (d) Kuandaa na kutekeleza mipango ya kuendelea kwa elimu na mafunzo ya majaji, mahakimu, maafisa wengine wa idara ya mahakama na wafanyakazi wengine katika kazi hiyo; na
  • (e) kuishauri Serikali ya Kitaifa kuboresha utendakazi na utekelezaji wa haki na pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kisheria.

(2) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume itaongozwa na yafuatayo–

  • (a) ushindani na utaratibu wenye uwazi katika kuwaajiri maafisa wa idara ya mahakama na wafanyakazi wengine katika idara hiyo.
  • (b) kukuza usawa wa kijinsia.