Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 174. Malengo ya Ugatuzi

Malengo ya Serikali ya ugatuzi ni–

  • (a) kuhakikisha kuwa kuna mamlaka ya kidemokrasia na uwajibikiaji wa Serikali;
  • (b) kuhimiza umoja wa kitaifa kwa kutambua uanuwai wa jamii mbalimbali;
  • (c) kuwapa watu katika kila ngazi mamlaka ya kujitawala na kushiriki katika matumizi ya mamlaka ya Serikali katika kufanya maamuzi ya mambo yanyowaathiri;
  • (d) kutambua haki za jamii zote katika kusimamia masuala ya jamii zao na kujiendeleza zaidi;
  • (e) kulinda na kuhamasisha maslahi na haki za jamii za watu walio wachache na zile za watu waliotengwa;
  • (f) kustawisha miradi ya kijamii na kiuchumi na utoaji wa huduma za karibu na zilizo rahisi ili kumfikia kila mtu nchini Kenya;
  • (g) kuhakikisha kuna ugavi sawa wa rasilmali zote za kijamiina za kitaifa kote nchini.
  • (h) kufanikisha ugatuzi wa mamlaka ya taasisi za Serikali, uendeshaji wake wa shughuli ama huduma kutoka mji mkuu wa Kenya; na
  • (i) kuhakikisha kuna kudhibiti na kugawana mamlaka kwa njia iliyo sawa.