Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

29. Uteuzi Mpya

(1) Utaratibu wa uteuzi wa watu wa kujaza nafasi zitakazopatikana kutokana na kutekelezwa kwa Katiba hii, utaanza tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hiyo na kukamilika katika kipindi cha mwaka mmoja.

(2) Isipokuwa pale ambapo Mpangilio huu ueleze kinyume, wakati Katiba hii itakapohitaji uteuzi ambao hauna budi kufanywa na Rais na kuidhinishwa na Baraza Kuu la Kitaifa, hadi baada ya uchaguzi wa kwanza chini ya Katiba hii, kwa mujibu wa Sheria ya Muafaka wa Kitaifa na Maridhiano, Rais atamteua mtu baada ya kushauriana na Waziri Mkuu kwa idhini ya Baraza Kuu la Kitaifa