Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

30. Uraia Kwa Kuzaliwa

Raia wa Kenya ni raia kwa kuzaliwa iwapo–

  • (1) amepata uraia chini ya kifungu cha 87 au 88 (1) cha Katiba ya awali; au
  • (2) angepata uraia kama kifungu cha 87 (2) kingesomwa:
    “Kila mtu ambaye alizaliwa nje ya Kenya, na mnamo tarehe 11-Disemba, 1963 ni raia wa Uingereza na Koloni zake au mtu aliyepata ulinzi wa Uingereza atakuwa, iwapo mamake au babake atakuwa , au angekuwa lakini kwa sababu ya kifo cha mmoja au wote wamekuwa, raia wa Kenya kwa sababu ya ibara ndogo ya (1), atakuwa raia wa Kenya mnamo tarehe 12 Disemba, 1963.”