25. Tume za Kikatiba
Tume ya Mishahara na Kuzawidi itaundwa katika miezi tisa baada ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii.
Tume ya Mishahara na Kuzawidi itaundwa katika miezi tisa baada ya tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba hii.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu atakuwa mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Usawa kwa kipindi cha kudumu cha wadhifa wake.
Tume ya Mipaka iliyobuniwa chini ya Katiba ya awali itaendelea kuhudumu kama ilivyoundwa katika Katiba hiyo.
Wakati wanachama wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka watakapoteuliwa, haja ya mwendelezo na kuhifadhi ujuzi na tajiriba itazingatiwa.
Utaratibu wa uteuzi wa watu wa kujaza nafasi utaanza tarehe ya kutekelezwa kwa Katiba na kukamilika kwa mwaka mmoja.