Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

26. Tume ya Haki za Binadamu na Usawa

(1) Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Usawa walioteuliwa chini ya Sheria ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Kenya ya mwaka wa 2002 ( Na. 9 ya 2002) na makamishna wa Tume ya Kitaifa ya Jinsia na Maendeleo iliyoteuliwa chini ya Sheria ya mwaka wa 2003 (Na. 13 ya 2003), mbali na Makatibu Wakuu na Mwanasheria Mkuu au mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu, watakuwa wanachama wa Tume ya Haki za Binadamu na Usawa wa kudumu lakini kila mmoja wao atabakia na kanuni zake za utendakazi wakati wa kutekelezwa kwa Katiba hii.

(2) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu atakuwa mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Usawa kwa kipindi cha kudumu cha wadhifa wake naye mwenyekiti wa Tume ya Jinsia na Maendeleo atakuwa Naibu – Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Usawa kwa kipindi cha kudumu kama vile mwenyekiti katika wadhifa wake.