1. Ufasiri
Katika Mpangilio huu, isipokuwa tu muktadha uonyeshe vinginevyo, "Tume ya Mipaka" inamaanisha Tume Huru ya Muda ya Mipaka.
Katika Mpangilio huu, isipokuwa tu muktadha uonyeshe vinginevyo, "Tume ya Mipaka" inamaanisha Tume Huru ya Muda ya Mipaka.
Masharti ya Katiba hii yanayohusu serikali ya ugatuzi yamesimamishwa hadi tarehe ya uchaguzi wa kwanza.
Hadi pale Bunge litakapopitisha Sheria inayotarajiwa katika Vifungu vya 15 na 18, sehemu ya 93 ya Katiba ya awali inaendelea kutumika.
Kutakuwa na kamati teule ya Baraza la Kitaifa itakayojulikana kama Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Katiba.
Tume ya Utekelezaji wa Katiba imeundwa.