Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

4. Kamati Teule ya Bunge

Kutakuwa na kamati teule ya Baraza la Kitaifa itakayojulikana kama Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Katiba itakayowajibikia kusimamia utekelezaji wa Katiba hii, na ambayo, miongoni mwa vitu vingine–

 • (a) Itapokea ripoti za kila mara kutoka kwa Tume ya Utekelezaji wa Katiba ikiwa ni pamoja na ripoti kuhusu–
  • (i) Kuandaa sheria inayohitajika na Katiba hii na changamoto zozote kuihusu;
  • (ii) Hatua za kuunda tume mpya;
  • (iii) Hatua ya kuunda miundo misingi inayohitajika kutekeleza shughuli za kila kaunti kwa njia mwafaka pamoja na hatua za kutambua afisi na mabaraza pamoja na kuajiri na kuhamisha wafanyikazi.
  • (iv) Ugatuzi wa mamlaka na majukumu kwa kaunti chini ya sheria iliyozingatiwa katika sehemu ya 15 ya Mpangilio huu; na
  • (v) vizuizi vyovyote katika hatua za utekelezaji wa Katiba hii.
 • (b) Kushirikiana na Mwanasheria Mkuu, Tume ya Utekelezaji wa Katiba na kamati husika za Bunge kuhakikisha sheria inayohitajiwa na Katiba hii imewasilishwa na kupitishwa kwa wakati ufaao; na
 • (c) Kuchukua hatua mwafaka za ripoti ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo yoyote katika utekelezaji wa Katiba hii.