Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 132. Majukumu ya Rais

(1) Rais ata–

  • (a) toa hotuba katika ufunguzi wa kila Bunge jipya lililoteuliwa;
  • (b) toa hotuba katika kikao maalumu cha Bunge mara moja kwa mwaka na anaweza kuhutubia Bunge wakati mwingine wowote.
  • (c) Mara moja kila mwaka–
    • (i) atoe ripoti, kupitia kwa hotuba kwa taifa, kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na maendeleo ambayo yamepatikana ili kufikia uadilifu wa kitaifa uliotajwa katika Kifungu cha cha 10;
    • (ii) kuchapisha katika Gazeti Rasmi la Serikali, yaliyomo katika hatua na maendeleo yaliyoelezewa katika sehemu ya aya (i); na
    • (iii) kuwasilisha ripoti kwa Baraza la Kitaifa ili kujadiliwa kuhusu mafanikio ambayo yamepatika katika utimizaji wa majukumu ya kimataifa ya Jamhuri.

(2) Rais atapendekeza na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa, ateue na anaweza kuwaachisha kazi–

  • (a) Mawaziri kwa mujibu wa Kifungu cha 152;
  • (b) Mwanasheria Mkuu kwa mujibu wa Kifungu cha 156;
  • (c) Katibu wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa Kifungu cha 154;
  • (d) Makatibu wakuu kwa mujibu wa Kifungu cha 155;
  • (e) Mabalozi, wanadiplomasia, maafisa wa balozi na wawakilishi wengine wa nchi; na
  • (f) Kwa mujibu wa Katiba hii, afisa yeyote mwingine wa taifa au wa umma ambaye Katiba hii inamtaka au kumpa Rais uwezo wa kumteua au kumwachisha kazi.

(3) Rais-

  • (a) ataongoza mikutano ya Baraza la Mawaziri;
  • (b) ataelekeza na kuratibu majukumu ya wizara na idara za serikali; na
  • (c) kwa uamuzi uliochapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali, atagawa majukumu kwa Mawaziri ili kutekeleza na kutawala Sheria yoyote ya Bunge na si kwa kiasi ambacho hakiambatani na Sheria yoyote ya Bunge.

(4) Rais anaweza–

  • (a) kutekeleza jukumu lolote la kiserikali lililoelekezwa katika Katiba hii au katika sheria ya kitaifa na, isipokuwa vinginevyo, kama ilivyoelekezwa katika, Katiba hii kubuni afisi katika huduma ya umma kwa mapendekezo ya Tume ya Huduma ya Umma;
  • (b) kupokea mabalozi na wawakilishi wa balozi za nchi za nje;
  • (c) kutunukia heshima kwa jina la watu na Jamhuri;
  • (d) kulingana na Kifungu cha 58, kutangaza hali ya hatari; na
  • (e) kwa idhini ya Bunge, anaweza kurangaza vita.

(5) Rais atahakikisha kwamba majukumu ya kimataifa kwa Jamhuri yanatimizwa kupitia kwa utendaji wa Mawaziri husika.