Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 131. Mamlaka ya Rais

(1) Rais–

  • (a) ndiye Kiongozi wa Taifa na Serikali;
  • (b) anatekeleza mamlaka makuu ya Jamhuri kwa usaidizi wa Naibu wa Rais na Mawaziri;
  • (c) ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Kenya;
  • (d) ndiye mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Usalama
  • (e) ni ishara ya umoja wa kitaifa.

(2) Rais–

  • (a) ataiheshimu, kuifuata na kuilinda Katiba;
  • (b) ataulinda uhuru wa Jamhuri ya Kenya.
  • (c) atakuza na kudumisha umoja wa taifa.
  • (d) atakuza heshima ya uanuwai wa watu wa Kenya; na
  • (e) kuhakikisha ulinzi wa uhuru na haki za kimsingi za raia na utawala wa sheria.

(3) Rais hatasimamia afisi nyingine yoyote ya Serikali au ya umma.