Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 98. Uanachama wa Seneti

(1) Seneti itajumuisha–

  • (a) wanachama arobaini na saba, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na wapigakura waliosajiliwa kwenye kaunti, na kila kaunti ikiwa ni eneowakilishi la mwanachama mmoja;
  • (b) wanachama wanawake kumi na sita watakaoteuliwa na vyama vya kisiasa kulingana na usawa wao wa wanachama kwenye Seneti waliochaguliwa chini ya ibara ya (a) kwa mujibu wa Kifungu cha 90;
  • (c) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja ili kuwakilisha vijana;
  • (d) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja wakiwakilisha watu wenye ulemavu; na
  • (e) Spika atakayekuwa mwanachama m’badala kwa mujibu wa wadhifa wake.

(2) Wanachama waliotajwa katika ibara ya (1) (c) na (d) watachaguliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 90.

(3) Hakuna chochote katika Kifungu hiki kitafasiriwa kama kinachomuondoa mtu yeyote katika ugombeaji wa uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a).