Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 246. Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa

(1) Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa imeundwa.

(2) Tume inahusisha–

  • (a) watu wafuatao, kila mmoja wao akiwa ameteuliwa na Rais-
    • (i) mtu anayestahili kuteuliwa kama Jaji wa Mahakama ya Juu;
    • (i) maafisa wawili wa polisi wa ngazi za juu waliostaafu; na
    • (ii) watu watatu wenye maadili mema ambao wamewahi kuhudumu serikalini kwa umahiri mkubwa.
  • (b) Inspekta-Mkuu wa Huduma za Polisi za Kitaifa.
  • (c) Manaibu wote wawili wa Inspekta-Mkuu wa Huduma za Polisi za Kitaifa.

(3) Tume–

  • (a) itaajiri na kuteua watu kuhudumu au kushikilia kwa muda afisi za huduma hiyo, kuidhinisha uteuzi na kuamua watakaopandishwa vyeo na kuhamishwa katika huduma za polisi za kitaifa.
  • (b) itazingatia utaratibu wa sheria, kutekeleza majukumu ya kinidhamu na kuwaondoa watu wanaohudumu au kushikilia kwa muda afisi za huduma hii; na
  • (c) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa sheria ya nchi..

(4) Uajiri katika Huduma za Polisi za Kitaifa utabainisha tofauti za kimaeneo na za jamii mbalimbali za watu wa Kenya.