Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 181. Kuondolewa kwa Gavana wa Kaunti

(1) Gavana wa kaunti anaweza kuondolewa kutoka afisini katika msingi wowote kati ya misingi ifuatayo–

  • (a) ukiukaji wa katiba hii au sheria yoyote uliokithiri;
  • (b) ikiwa pana sababu ya kutosha kuamini kuwa gavana huyo wa kaunti amefanya uhalifu chini ya sheria ya taifa au kimataifa;
  • (c) kutumia mamlaka ya afisi vibaya au utovu wa nidhamu uliokithiri;
  • (d) kukosa uwezo wa kimwili au kiakili kutekeleza majukumu ya afisi ya gavana.

(2) Bunge litatunga sheria ya kutoa kanuni za kufuatwa kumuondoa gavana afisini kwa msingi wowote uliotajwa katika ibara ya (1).