Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 178. Spika wa Baraza la Kaunti

(1) Kila baraza la kaunti litakuwa na spika aliyechaguliwa na baraza la kaunti kutoka kwa watu wasio wanachama wa baraza hilo.

(2) Kinara wa kikao cha baraza la kaunti atakuwa–

  • (a) spika wa baraza hilo; au
  • (b) wakati spika hayupo, mwanachama mmoja aliyeteuliwa na baraza hilo.

(3) Baraza litatunga sheria itakayoruhusu kuchaguliwa na kuondolewa afisini kwa maspika wa mabaraza ya kaunti.