Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 18. Sheria Kuhusu Uraia

Bunge litaunda sheria–

  • (a) kueleza taratibu ambazo kupitia kwazo mtu anaweza kuwa raia;
  • (b) kuongoza uingiaji na kukaa nchini Kenya
  • (c) kutoa hali ya wakaazi wa kudumu;
  • (d) kutoa nafasi ya kukana uraia kwa hiari;
  • (e) kutoa taratibu za kupokonywa uraia;
  • (f) kuamua majukumu na haki za raia; na
  • (g) Kwa jumla, kuyawezesha masharti ya Sura hii.