Kifungu 156. Mwanasheria Mkuu
Mwanasheria Mkuu atapendekezwa na Rais na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa, kuteuliwa na Rais.
Kifungu 157. Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atapendekezwa na Rais, na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa, atateuliwa na Rais.
Kifungu 158. Kuondolewa na Kujiuzulu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma
Mkurugezi wa Mashtaka ya Umma, ambaye amesimamishwa kazi atapokea nusu ya mshahara hadi wakati wa kuachishwa kazi au kurudishwa kazini.