Kifungu 163. Mahakama ya Juu
Mahakama ya Juu itakuwa imebuniwa kisawasawa kwa minajili ya kesi zake iwapo itakuwa na majaji watano.
Kifungu 164. Mahakama ya Rufani
Kutakuwa na Rais wa Mahakama ya Rufaa ambaye atachaguliwa na majaji wa mahakama ya Rufaa kutoka miongoni mwao.
Kifungu 165. Mahakama Kuu
Kutakuwa na Jaji Kinara wa Mahakama Kuu ambaye atachaguliwa na majaji wa mahakama ya Juu kutoka miongoni mwao.
Kifungu 166. Uteuzi wa Jaji Mkuu, Naibu wa Jaji Mkuu na Majaji Wengine
Rais atateua Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu kulingana na mapendekezo ya Tume ya Huduma ya Mahakama.
Kifungu 167. Kipindi cha Kudumu Afisini kwa Jaji Mkuu na Majaji Wengine
Jaji Mkuu na jaji mwingine yeyote anaweza kujiuzulu kutoka afisini kwa kuandika barua kwa Rais.
Kifungu 168. Kuondolewa kutoka Afisini
Hatua ya kumuondoa jaji kwenye wadhifa wake inaweza kuanzishwa na Tume ya Huduma za Mahakama.