Kifungu 159. Mamlaka ya Mahakama
Mamlaka ya Mahakama yanatokana na watu, yanajikita katika mahakama na mahakama maalum zinazobuniwa kulingana na Katiba hii.
Kifungu 160. Uhuru wa Mahakama
Afisi ya jaji wa mahakama ya Mamlaka Kuu haitafutiliwa mbali wakati ambapo kuna afisa anayeshikilia wadhifa huo.
Kifungu 161. Afisi na Maafisa wa Mahakama
Mahakama inahusisha majaji wa mahakama za mamlaka ya juu, mahakimu na maafisa wengine wa idara ya Mahakama.
Kifungu 162. Mfumo wa Mahakama
Mahakama za mamlaka ya juu ni Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu na mahakama nyingine.