Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Wajibu wa Msimamizi wa Uchaguzi nchini Kenya

  • Mwandishi Gĩthĩnji
  • Imesasishwa:

Jukumu la Msimamizi wa Uchaguzi nchini Kenya ni kuhakikisha kwamba uendeshaji wa uchaguzi unafuata sheria. Msimamizi wa Uchaguzi anatakiwa asiwe na upendeleo katika kutekeleza majukumu yake.

Msimamizi wa Uchaguzi ni mfanyakazi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.

Jukumu la Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ni kuendesha au kusimamia kura za maoni na uchaguzi wa chombo chochote cha kuchaguliwa au ofisi iliyoanzishwa na Katiba, na uchaguzi mwingine wowote kama ilivyoainishwa na Sheria ya Bunge.

Wajibu wa Msimamizi wa Uchaguzi ni (kawaida) katika eneobunge. Afisa Msimamizi katika Kituo ha kupigia kura anawajibika kwa Msimamizi wa Uchaguzi.

Jedwali la YaliyomoOnyesha/Ficha

Wajibu wa Msimamizi wa Uchaguzi nchini Kenya

Wajibu wa Msimamizi wa Uchaguzi nchini Kenya ni kama ifuatavyo–

  • hutangaza matokeo ya uchaguzi katika kitengo maalum cha uchaguzi;
  • hutia sahihi fomu rasmi za kutangaza matokeo;
  • hutuma matokeo rasmi kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha ikiwa mfumo wa upitishaji wa kielektroniki unatumika;
  • hupeleka fomu rasmi ya matokeo ya uchaguzi kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha;
  • hutangaza mshindi katika kitengo fulani cha uchaguzi;
  • hutia sahihi na kutoa cheti rasmi kwa mshindi;
  • husimamia usajili, mafunzo na utumaji wa maafisa wa uchaguzi katika vituo vya uchaguzi;
  • huamua kura zinazobishaniwa.

Wajibu wa Naibu Msimamizi wa Uchaguzi

Wajibu wa Naibu Msimamizi wa Uchaguzi nchini Kenya ni kama ifuatavyo–

  • ndiye msaidizi rasmi wa Msimamizi wa Uchaguzi
  • hutekeleza majukumu aliyopewa na Msimamizi wa Uchaguzi
  • hutekeleza majukumu ya Msimamizi wa Uchaguzi ikiwa hayuko.

Sifa za Msimamizi wa Uchaguzi na Naibu Msimamizi wa Uchaguzi

Sifa za Msimamizi wa Uchaguzi na Naibu Msimamizi wa Uchaguzi ni pamoja na zifuatazo–

  • awe raia wa Kenya mwenye uadilifu wa hali ya juu, na asiyependelea upande wowote;
  • awe na cheti cha Shahada au Diploma kutoka katika taasisi inayotambulika;
  • awe na ujuzi wa kompyuta;
  • awe na mawasiliano madhubuti;
  • awe na ujuzi mzuri wa kuandika ripoti;
  • awe na uwezo wa kudhibiti watu, data nyeti na nyenzo;
  • awe na ujuzi katika kuhesabu data;
  • lazima awepo kwa kipindi chote cha Uchaguzi;
  • lazima awe mkaazi katika eneobunge na Wadi anayoomba kazi.
Makala Zaidi