Ruka hadi Yaliyomo
Bajeti

Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali za Kaunti

Mwaka wa Fedha wa 2019/2020

Lengo la jumla la mapato ya kila mwaka la kaunti katika Mwaka wa Fedha wa 2019/20 lilikuwa shilingi bilioni 54.9 ikilinganishwa na ukusanyaji halisi wa shilingi bilioni 35.77, ambazo zilikuwa asilimia 65.2 ya lengo.

Huu ulikuwa upungufu ikilinganishwa na shilingi bilioni 40.30 zilizozalishwa katika Mwaka wa Fedha wa 2018/19 (ambazo zilikuwa asilimia 74.8 ya lengo la mapato ya mwaka huo).

Kumbuka: Kiasi ni katika mamilioni ya shilingi za Kenya.

Kaunti Lengo la Mwaka Mapato Halisi Mapato Halisi/
Lengo la Mwaka
(%)
Baringo 393.42 301.66 76.7
Bomet 200.92 201.51 100.3
Bungoma 919.10 777.46 84.6
Busia 504.50 225.83 44.8
Elgeyo Marakwet 149.90 131.96 88
Embu 920.00 509.65 55.4
Garissa 150.00 109.92 73.3
Homa Bay 177.59 274.60 154.6
Isiolo 170.86 122.08 71.4
Kajiado 1,579.25 616.80 39.1
Kakamega 1,666.14 1,180.81 70.9
Kericho 711.64 473.73 66.6
Kiambu 3,540.85 2,466.26 69.7
Kilifi 1,100.00 788.78 71.7
Kirinyaga 480.00 374.74 78.1
Kisii 870.00 333.15 38.3
Kisumu 1,438.48 804.35 55.9
Kitui 600.00 408.29 68.0
Kwale 325.00 254.45 78.3
Laikipia 1,006.88 727.96 72.3
Lamu 100.00 108.91 108.9
Machakos 1,160.78 1,376.17 118.6
Makueni 655.24 644.48 98.4
Mandera 183.56 124.96 68.1
Marsabit 170.00 126.71 74.5
Meru 825.00 383.30 46.5
Migori 450.00 305.69 67.9
Mombasa 4,733.39 3,260.01 68.9
Murang'a 960.00 580.30 60.4
Nairobi City 17,347.14 8,715.07 50.2
Nakuru 3,100.00 2,551.21 82.3
Nandi 628.82 283.19 45.0
Narok 2,397.37 2,345.48 97.8
Nyamira 250.00 185.57 74.2
Nyandarua 630.00 379.48 60.2
Nyeri 1,000.00 664.86 66.5
Samburu 267.03 215.67 80.8
Siaya 420.00 179.43 42.7
Taita Taveta 230.00 296.04 128.7
Tana River 66.00 64.47 97.7
Tharaka Nithi 350.00 270.15 77.2
Trans Nzoia 500.00 356.08 71.2
Turkana 180.00 176.23 97.9
Uasin Gishu 900.00 779.33 86.6
Vihiga 192.09 148.20 77.2
Wajir 150.00 60.42 40.3
West Pokot 150.32 107.18 71.3
Jumla 54,901.27 35,772.58 65.2

Kuto 1 Julai 2019 mpaka 30 Juni 2020. Asili: Ripoti ya Msimamizi wa Bajeti ya 2019/20

Katika kipindi kinachoangaziwa, kaunti zilizopata kiwango cha juu zaidi cha mapato ya ndani zilikuwa–

  • Nairobi City kwa shilingi bilioni 8.72,
  • Mombasa kwa shilingi bilioni 3.26, na
  • Nakuru kwa shilingi bilioni 2.55.

Kaunti zilizozalisha kiasi cha chini zaidi zilikuwa–

  • West Pokot kwa shilingi milioni 107.18,
  • Tana River kwa shilingi milioni 64.47, na
  • Wajir kwa shilingi milioni 60.42.

Uchambuzi wa mapato ya ndani kama sehemu ya lengo la mapato ya kila mwaka unaonyesha kuwa kaunti tano zilivuka malengo yao ya mwaka, ambazo ni– Homa Bay, Taita Taveta, Machakos, Lamu na Bomet.

Kinyume chake, kaunti ambazo zilirekodi chini ya asilimia 50 dhidi ya malengo ya mwaka ni Meru, Nandi, Busia, Siaya, Wajir, Kajiado na Kisii.