Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Utangulizi

Sisi watu wa Kenya –

TUKITAMBUA utukufu wa Mungu Muumba wa vyote;
TUKIWAHESHIMU mashujaa wetu waliojitoa mhanga kupigania uhuru na haki kwa nchi yetu;
TUKIJIVUNIA tofauti zetu za kikabila, kitamaduni na kidini na kuazimia kuishi kwa amani na umoja tukiwa taifa moja dhabiti;
TUKITHAMINI mazingira yetu asili ambayo ndiyo urithi wetu na kuazimia kuyadumisha kwa manufaa ya vizazi vijavyo;
TWAJITOLEA kukuza na kuhifadhi maslahi ya watu binafsi, familia, jamii na taifa;
TWATAMBUA matarajio ya Wakenya wote kwa serikali iliyo na misingi bora ya haki za binadamu, usawa, demokrasia, haki za kijamii na utawala wa kisheria;
MATUMIZI ya uhuru wetu, haki yetu ya kuamua aina ya uongozi tuutakao na tukiwa tumeshiriki kikamilifu katika kuiunda katiba hii;
TUNAKUBALI, KUTEKELEZA, na kujipa sisi wenyewe na vizazi vijavyo, Katiba hii.

Mungu Ibariki Kenya