(1) Kutabuniwa afisi ya Katibu Mkuu ambayo ni afisi katika huduma ya umma.

(2) Kila Wizara au idara ya Serikali itakuwa chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu.

(3) Rais–

  • (a) atapendekeza mtu ili kuteuliwa kama Katibu Mkuu kutoka miongoni mwa wale waliopendekezwa na Tume ya Huduma za Umma; na
  • (b) atamteua Katibu Mkuu kwa idhini ya Baraza la Kitaifa.

(4) Rais anaweza kubadilisha au kumhamisha kazi Katibu Mkuu.

(5) Katibu Mkuu anaweza kujiuzulu kwa kumuandikia Rais notisi