Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 154. Katibu wa Baraza la Mawaziri

(1) Kuna afisi teule ya Katibu katika Baraza la Mawaziri ambayo ni afisi katika huduma za umma.

(2) Katibu katika Baraza la Mawaziri–

  • (a) atapendekezwa na Rais na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa kuteuliwa na Rais; na
  • (b) anaweza kuachishwa kazi na Rais.

(3) Katibu katika Baraza la Mawaziri–

  • (a) atakuwa na madaraka ya afisi ya Baraza la Mawaziri;
  • (b) atawajibika kulingana na maelekezo ya Baraza la Mawaziri, kwa kupanga shughuli na kuweka kumbukumbu za mikutano ya Baraza la Mawaziri;
  • (c) atawasilisha uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa watu au mamlaka zinazofaa; na
  • (d) atakuwa na majukumu kama itakavyoagizwa na Baraza la Mawaziri.

(4) Katibu katika Baraza la Mawaziri anaweza kujiuzulu kwa kutoa notisi ya maandishi kwa Rais.