Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 151. Malipo na Marupurupu ya Rais na Naibu wa Rais

(1) Mshahara na marupurupu yatakayolipwa Rais na Naibu wa rais yatatoka kwa Mfuko wa Jumla wa fedha.

(2) Malipo na marupurupu ya Rais na Naibu wa rais hayatabadilishwa kwa lengo la kutowanufaisha wakiwa afisini.

(3) Malipo ya uzeeni yanayopaswa kulipwa Rais mstaafu na Naibu wa rais mstaafu pamoja na marupurupu mengine wanayostahili hayatabadilishwa ili kutowanufaisha katika maisha yao yote.