Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 150. Kuondolewa kwa Naibu wa Rais

(1) Naibu wa rais anaweza kuondolewa mamlakani–

  • (a) kwa misingi ya kutokuwa na uwezo wa kiakili na kimwili wa kutekeleza majukumu ya kiafisi;
  • (b) kwa kura ya kutokuwa na imani–
    • (i) kwa misingi ya kukosa uwezo wa kimwili na kiakili wa kutekeleza majukumu ya afisi;
    • (ii) kwa sababu ya kuwa kuna sababu kubwa sana za kuamini kuwa Naibu Rais amefanya uhalifu wa jinai chini ya sheria za kitaifa ama kimataifa;
    • (iii) kwa utovu mkubwa wa nidhamu.

(2) Sheria katika Vifungu vya 144 na 145 vinavyohusiana na kuondolewa mamlakani kwa Rais, kukiwa na mabadiliko yanayostahili, itatumika katika kumuondoa Naibu wa rais.