Ruka hadi Yaliyomo
AfroCave

Kifungu 139. Kifo Kabla ya Kuchukua Mamlaka

(1) Iwapo aliyetangazwa kuwa Rais-mteule atafariki kabla ya kuchukua hatamu za uongozi–

  • (a) Naibu wa rais-mteule ataapishwa kama kaimu Rais siku ileile tu ambayo Rais mteule angeapishwa; na
  • (b) uchaguzi mpya wa Rais utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya kifo cha Rais-Mteule.

(2) Iwapo Naibu wa rais-mteule atafariki kabla ya kuchukua hatamu za uongozi, afisi ya Naibu wa rais itatangazwa kuwa wazi baada ya Rais-mteule kuchukua mamlaka.

(3) Iwapo Rais mteule pamoja na Naibu wa rais watafariki kabla ya kuchukua mamlaka–

  • (a) Spika wa Baraza la Kitaifa atakuwa kaimu Rais kuanzia siku ambayo Rais mteule angeapishwa; na
  • (b) uchaguzi mpya utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya kifo cha pili.