(1) Rais atachaguliwa na wapigakura waliosajiliwa katika uchaguzi wa kitaifa utakaoendeshwa kwa mujibu wa Katiba hii na Sheria nyingine yoyote ya Bunge inayothibiti uchaguzi wa Rais.

(2) Uchaguzi wa Rais utafanyika–

  • (a) siku moja na ile ya uchaguzi mkuu wa Wabunge, ikiwa ni siku ya Jumanne ya pili ya mwezi Agosti ya kila mwaka wa tano; au
  • (b) katika hali ambazo zinatajwa kwenye Kifungu cha 146.